Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi amewasamehe wafungwa kadhaa akiwemo mwanaharakati mashuhuri Ahmed Douma.
Douma, ambaye aliongoza maandamano ya kutetea demokrasia yaliyomuondoa madarakani rais Hosni Mubarak mwaka 2011, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mwaka 2019 kwa kufanya vurugu na kuwashambulia maafisa wa usalama.
Akitoa hukumu yake wakati huo, Jaji alisema Douma alikuwa miongoni mwa umati wa watu waliovamia Bunge na kuharibu sehemu ya jengo hilo.
Kama ilivyo kwa Wanaharakati wengine kadhaa nchini Misri, Douma pia alifungwa jela chini ya utawala wa Mubarak, uongozi wa baraza la kijeshi uliofuata, chini ya utawala wa rais wa zamani Mohamed Mursi, na rais wa sasa al-Sisi.