Rais John Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na kumteua Phillip Mpango kukaimu nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais amemtaka Bade kuhakikisha anashirikiana na Mpango katika kutafuta ukweli kuhusu makontena 349 yenye thamani ya shilingi bilini 80 yaliyotoweka bandarini bila TRA kuwa na kumbukumbu zozote.

Uamuzi huo wa rais umekuja saa chache baada ya waziri mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kubaini kutokuwepo kwa taarifa za makontena hayo 349 kwenye nyaraka za TRA huku taarifa hizo zikionekana kwenye nyaraka za Bandari.

Waziri Mkuu aliwasimamisha maafisa kadhaa na kumrisha baadhi yao kukamatwa ili kuhakikisha ukweli unawekwa wazi na wahusika wote wanachukuliwa hatua.

Tyson Kurejea Ulingoni Wikiendi Hii
Harakati Za Kumsaka Bingwa Wa SDL Kuendelea Kesho