Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametangaza muda wa wananchi kukaa karantini umeongezwa kwa wiki mbilili mbele kwa lengo la kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona vilivyoenea nchini humo.

Alipokuwa anatangaza ongezeko hilo amesema, zikiwa siku 21 za awali zinakaribia kuisha ni hatari sana kuwaacha watu wakatoka kabla maambukizi ya ndani hayajakoma kwani watashindwa kuhudumia wote.

Nchi hiyo ambayo imeendelea kiuchumi barani Afrika, ina visa 1,934 vya waathirika wa corona na inakadiriwa kuwa wanaweza kuongezeka zaidi kadri vipimo vinavyoendelea kuchukuliwa.

Wananchi wa Afrika Kusini walianza kukaa ndani Machi 27 baada ya maambukizi kusambaa kwa kasi ambapo hadi sasa duniani kuna visa zaidi ya milioni 1.5 na vifo zaidi ya elfu 90 duniani kote.

Antonio Nugaz: Uongozi, GSM wametuonyesha njia
Video: Wananchi wote kuvaa barakoa, Ni pasaka ya aina yake