Rais wa Ghana, John Mahama amepiga marufuku safari za ndege kwa tiketi ya daraja la kwanza kwa watumishi wa umma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kubana matumizi.

Rais wa Ghana, John Mahama

Rais wa Ghana, John Mahama

Taarifa ya serikali ya nchi hiyo iliyotolewa wiki hii imeeleza kuwa hatua hiyo imekuja wakati ambapo nchi hiyo inapambana kubana matumizi yasiyo ya lazima huku wakitumia msaada wa IMF kujiimarisha kiuchumi.

“Rais ametoa maagizo hayo wiki hii akiwataka mawaziri wote na maafisa waandamizi kuhakikisha wanaepuka safari za nje ya nchi zisizo za lazima na siziso na kibali maalum,” Waziri wa Mawasiliano, Edward Omane aliwaambia waandishi wa habari.

 

Somalia Yafuta Sherehe za Krismas
Magufuli Amfyeka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Avunja Bodi Mbili