Serikali nchini Sierra Leone, imepitisha sheria inayolazimisha mashirika ya umma na kibinafsi kutenga asilimia 30 ya kazi zao kwa ajili ya wanawake, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika jamii inayopendelea wanaume.
Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio tayari amesaini mswada huo kuwa sheria, ambao pia unawahakikishia wanawake angalau wiki 14 za likizo ya uzazi, malipo sawa na fursa za mafunzo kazini.
Mara baada ya kusaini muswada huo, Rais Bio amesema anatarajia sheria hiyoitashughulikia ipasavyo ukosefu wa usawa wa kijinsia katika nchi na kwamba watahakikisha kuwa inafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Nchini Sierra Leonne, Wanawake wanakabiliwa na ubaguzi wa kimfumo, huku Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, likisema ni jambo la kawaida kuwafuta kazi wanawake iwapo watashika ujauzito.