Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewatembelea wafanyabiashara mbalimbali wa maduka ya vyakula ya rejareja.

Ziara hiyo ya kushtukiza, ilikuwa na lengo la kujionea hali ya chakula ilivyo na bei zake katika eneo la Chake Chake Pemba hii leo Februari 12, 2023.

Aidha, Rais Mwinyi pia alipata wasaa wa kupokea maelezo kutoka kwa wafanyabishara hao, kuhusiana na bei za vyakula na upatikanaji wake.