Rais wa Mexico, Enrique Peña amesema amefedheheshwa na taarifa alizozipata kuhusu tajiri muuza unga nguli anaefahamika kwa jina la El Chapo Guzman, kutoroka mara ya pili jela yenye ulinzi mkali zaidi nchini humo.

Akiongea na waandishi wa habari Jumapili iliyopita akiwa nchini Ufaransa, rais Pena alisema kuwa amekuwa akifuatilia kwa karibu habari kuhusu tukio hilo la kutoroka kwa mtu huyo ambaye ni mharifu anaetafutwa zaidi na nchi hiyo.

Alisema tukio hilo limemfehesha sana na ni pigo kwa nchi na jamii ya watu wa Mexico kwa ujumla. Aliongeza kuwa serikali ya nchi hiyo inafanya uchunguzi wa kina kuona kama kuna mfanyakazi yeyote wa jela hiyo aliyemsaidia ‘don’ huyo wa madawa ya kulevya kuutoroka ulinzi mkali wa kisasa ulioko katika jela hiyo.

“Nina uhakika kuwa taasisi za nchi ya Mexico, hususan vyombo vyenye jukumu la usalama wa umma, viko kwenye nafasi nzuri, vina nguvu na utambuzi wa kumkamata tena mtu huyo,” alisema rais huyo.
El Chapo Guzman ni tajiri mkubwa, kati ya maboss wakubwa zaidi wa mtandao wa madawa ya kulevya duniani wanaofanya biashara hiyo kwa njia za hatari.

Guzman aliyekamatwa mwaka 2014, alitoroka jela hiyo huku kamera zikiinasa sura yake kwa mara ya mwisho Jumamosi, muda mchache kabla ya kupenya vizingiti na kutambaa katikati ya mfereji wa maji unaotokea baharini.

Hii ni mara ya pili kwa Guzman kutoroka jela ambapo mwaka 2001 pia alitoroka kwa mtindo wa aina yake. Ingawa vyombo vya usalama vya nchi hiyo vilimtafuta usiku na mchana, ilivichukua takribani miaka 13 kufanikisha zoezi hilo. Walimkamata katika eneo la hotel ya kifahari kwenye ufukwe wa bahari nchini humo.

Raila Odinga Aeleza Kenya Ilivyopokea Ushindi Wa Magufuli Na Kama Aliwahi Kumgusia Kuutaka Urais
Abakwa Mara Ya Pili Baada Ya Polisi Kumtumia Kama Mtego Kuwakamata Wabakaji