Rais wa Tunisia Kais Saied ametangaza kuvunja bunge la nchi hiyo na kumtimua kazi waziri mkuu wa nchi hiyo Hichem Mechichi
Hatua hii imekuja baada ya siku moja ya maandamano na vurugu za kupinga mpango wa serikali na chama tawala nchini humo kuhusu janga la Corona.
Waandamanaji waliishtumu serikali ya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika kuwa imeshindwa kuwa na mkakati imara wa kushughulika na virusi vya Corona huku wakikosoa uamuzi wa kujifungia kwa kisingizio cha kuepusha na maambukizi zaidi.
Ras Kais ameamua kuchukua hatua haraka kabla ya maandamano hayo yaliyokusanya maelfu ya watunisia hayajaenda mbali zaidi na kuahidi mabadiliko ya sera