Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amewafuta kazi mawaziri sita akiwemo waziri wa fedha.
Tangazo hilo lilitolewa katika taarifa ambayo haikutoa sababu zozote za kufukuzwa kazi kwa mawaziri hao wala kutoa dalili za lini nafasi hizo zitapewa watu wengine.
Haya ni mabadiliko ya pili makubwa ya baraza la mawaziri katika miezi ya hivi karibuni.
Wengine waliofutwa kazi ni pamoja na waziri wa rasilimali za madini na nishati, bahari, maji na uvuvi na kazi za umma, nyumba na rasilimali za maji.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini walisema hawakushangazwa na kufukuzwa kazi kwa watumishi hao.
Mnamo Novemba, Rais Nyusi aliwaachisha kazi waziri wa ulinzi na mambo ya ndani na kueka wengine.