Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amezindua mradi wa kilimo uliopewa jina la “Mega Farms” unaolenga kuimarisha uchumi wa Kilimo wa Taifa hilo na kumaliza uhaba wa chakula unaoshuhudiwa mara kwa mara.

Malawi imekuwa ikishuhudia uhaba wa chakula licha ya juhudi nyingi za kuongeza uzalishaji ikiwepo program ya Targeted Inputs, inayotoa mbegu na mbolea za bei nafuu kwa wakulima.

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera akiwa Shambani. Picha ya Ikulu ya Malawi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwezi jana (Agosti), umesema Takriban watu milioni 4.4 wa Malawi ambao ni sawa na asilimia 22 ya jumla ya wakazi nchini humo, wana uhaba wa chakula, wakati hali hiyo ikitarajiwa kuongezeka kuanzia Oktoba 2024.

Akizungumza kwa njia ya televisheni wakati wa uzinduzi wa mradi huo mpya, Rais Chakwera amesema analenga kuongeza fedha za kigeni nchini humo, pamoja na kuhakikisha Taifa linajikimu kwa chakula.

Djuma Shabani kumng'oa mtu Azam FC
Waendesha Bodaboda warudishwa katika mstari