Rais wa Sudan, Omar Bashir amevunja Baraza lake la Mawaziri na kumchagua Waziri mkuu mpya ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi ulioikumba nchi yake.

Amemteua Motazz Moussa kuwa Waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, ambaye anashika nafasi ya Bakri Hassan Saleh aliyechaguliwa kuongoza nafasi hiyo mwaka 2017.

Aidha, kabla ya kuteuliwa katika nafasi yake hiyo, Motazz Moussa alikuwa ni Waziri anayeshughulikia masuala ya umeme na umwagiliaji.

Uamuzi huo umekuja mara tu baada ya Rais Omar Bashir kuitisha kikao cha dharura cha maafisa wa chama tawala katika makazi yake katika kipindi ambacho wasiwasi wa hali ya kiuchumi imekuwa ikiongezeka kutokana na kupanda bei za vitu na vingine kutopatikana.

Hata hivyo, awali Naibu Mwenyekiti wa chama tawala nchini humo cha National Congress Faisal Hassan amewaambia waandishi wa habari kwamba Mawaziri wa Mambo ya Nje, Ulinzi na masuala ya Rais watabaki katika nafasi zao, mpaka litakapoundwa baraza jipya la mawaziri.

Mke wa Mugabe aeleza ‘wema’ aliofanyiwa na Rais Mnangagwa
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma Septemba 10, 2018