Rais wa Marekani Joe Biden leo atatembelea mji wa Poland ambao uko karibu na mpaka na Ukraine, kwa lengo la kuonesha mshikamano na Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi
Katika eneo hilo la Rzesow, lililo umbali wa kilometa 50 kutoka mpakani mwa Ukraine, Biden atakutana na Rais wa Poland, Andrzej Duda, hii ni safari yake ya dharura barani Ulaya ambayo imesababishwana vita vya Ukraine.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema katika ziara yake ya Machi 5 alilitembelea eneo hilo kwa lengo la kuonesha uungaji wake mkono kwa wanajeshi wa NATO, kwa iliyokuwa seheumu ya Jumuiya ya Kisovieti.
Ikulu ya Marekani inasema katika ziara hiyo, Biden atapokea taarifa ya namna gani Poland inakabiliana na wimbi la mamilioni ya wakimbizi ambao wanakimbia makombora ya Urusi huko Ukraine. Aidha atakutana na wanajeshi wa kikosi cha anga ambao wana kambi yao katika eneo hilo la Rzeszw.
Katika hatua nyingine afisa wa ngazi ya juu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani Colin Kahl amesema vita vya Ukraine vimeibebesha China jukumu zito katika mahusiano yake na Urusi. Amesemna anadahani kuna kiwango cha mambo kinachofanywa na Urusi nchini Ukraine ambacho kimefanya jambo hilo kuwa gumu kwa China, kuliko ilivyokuwa wiki sita iliyopita au miezi sita.
Mwezi Februari, China na Urusi zilitangaza uhusano usio na kikomo, katika kuungana mkono katika mizozo ya Ukraine na Taiwan, na kushirikiana zaidi dhidi ya mataifa ya Magharibi.
Wabunge wa Ukraine jana Alhamisi wamepiga kura kumwadhibi yeyote anaisaidia Urusi akiwa ndani ya taifa hilo kuhukumiwa kifungo hadi cha miaka 12 gerezani. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya bunge la taifa hilo vitendo hivyo ni pamoja na kuunga mkono, kusafirisha fedha na usaidizi wowote kwa jeshi la Urusi.
Pamoja na adhabu ya kifungo, mtu atakaekutwa na hatia pia atazuiwa kufanya kazi serikalini katika kipindi cha miaka 15 na mali zake kutaifishwa.