Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amechangia shilingi milioni kumi na tano kwa ajli ya kumaliza ujenzi wa Zahanati ya Mnolela katika jengo ambalo limejengwa kwa  nguvu za wananchi kwa kiasi cha shilingi milioni 40.

Rais Magufuli ametoa msaada huo wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Mtwara ambapo  alisimama katika kata ya Mnolela kuzungumza na wananchi huku Mbunge wa Jimbo hilo, Nape Nnauye alipomuomba Rais kumalizia Jengo hilo kwani baadhi ya kina mama hujifungulia nje kutokana na uhaba wa vyumba vya kujifungulia.

Aidha baada ya kupewa taarifa hiyo Rais Magufuli alikwenda kukagua jengo hilo ndipo alipoamuawa kuchangia  milioni kumi na tano huku Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ikichangia milioni 30 na Mbunge wa Jimbo la Mtama akichangia sh. milioni kumi na kuwashukuru wananchi hao kwa hatua hiyo.

Kwa upande wao wananchi  wa Mnolela wamemshukuru Rais Magufuli kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha kumalizia ujenzi huo ili kuweza kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo, Rais Magufuli amelazimika kusimama katika Kata ya Madangwa na kutoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa waLindi, Godfrey Zambi kuwashughulikia waliowadhulumu wakulima.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 5, 2017
Video: Furahia Wikendi na MIX ya video kali zilizotikisha miaka ya ‘kati’ na DJ Jors Bless