Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu.
Picha namba 5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo ya Mwigumbi-Maswa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa TAMISEMi na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri wakimwagilia maji mti mara baada ya kuupanda baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye Ubao kwa kutumia Chaki zinazotengenezwa na Kiwanda cha Chaki cha Maswa Mkoani Simiyu. Rais Dkt. Magufuli aliwapongeza wenye kiwanda hicho na kuwashauri kukipanua zaidi ili kiweze kuwafikia Watanzania wengi wenye mahitaji ya Chaki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakazi wa Maganzo mkoani Shinyanga mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Maswa mara baada ya kumaliza kuwahutubia Wilayani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka wakiangalia utengenezwaji wa Chaki katika kiwanda cha Chaki cha Maswa mkoani Simiyu. PICHA NA IKULU