Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wanaCCM kujibu hoja kwa vitendo badala ya maneno kwani wanadhima kubwa ya kuendeleza amani iliyopo nchini.
 
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Machi 27, 2022 katika ukumbi wa CCM Amani Mkoa, katika uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wazazi Tanzania, ambalo kitaifa mwaka huu linafanyika Zanzibar.
 
Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba hivi karibuni wametoa baadhi ya watu kuanza maneno maneno juu yake na Serikali anayoiongoza na kusema kwamba ni vyema watu hao wakajibiwa kwa vitendo badala ya maneno.
 
Rais Dk. Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, aliwataka wanaCCM kuwa na subira huku Serikali anayoiongoza ikitekeleza majukumu yake ipasavyo sambamba na chama chao kikiendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa vitendo.

Poland yaichokonoa Urusi
Simba SC yaomba mashabiki 10,000 CAF