Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Dkt. Said Khamis Juma kuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika Ikulu Zanzibar hii leo Juni 10, 2023 kabla ya kuanza kikao cha Tume ya Mipango.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameendelea kuweka msisitizo katika kuimarisha utawala bora, uwazi, na uwajibikaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lengo likiwa ni kuhakikisha ufanisi wa matumizi ya rasilimali za umma.

Dkt.Said Khamis Juma Naibu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali atamsaidia Dkt.Othman Abbas Ali Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanafanyika kwa uwazi, ufanisi, na kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo.

Azam FC kumng'oa Peter Banda Simba SC
Young Africans yatamba kutetea ASFC