Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara – TNBC, uliofanyika Ikulu Dar es Salaam hii leo Juni 9, 2023.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara – TNBC, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha, katika mkutano huo Mwenyekiti wa TNBC, Rais Dkt. Samia ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sera ya uchumi wa buluu na kuendelea kukuza soko la mazao ya bahari Duniani.

Aidha, pia amemshukuru Rais Dk.Mwinyi kwa kuhudhuria kwake mkutano huo na viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

TNBC iimarishe uwezo sekta binafsi - Rais Dkt. Samia
Wadaiwa kuuza chakula cha msaada, wahisani wasitisha huduma