Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwanzilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air, Michael Ngaleku Shirima.

Mfanyabiashara huyo amehudumu kwa karibu miaka 30 katika biashara ya anga na taarifa za kifo chake zimetolea mapema leo Juni 10.

Mwanzilishi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air, Michael Ngaleku Shirima.

Taarifa iliyochapishwa na @ikulu_mawasiliano imeeleza kuwa Rais Dkt. Samia amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo na kumuelezea kuwa alikuwa sehemu muhimu katika biashara ya anga na shughuli za kijamii nchini.

“Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina.” Ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Watatu wasajiliwa Simba SC kimya kimya
Joash Onyango: Azam FC imetuvurugia Simba SC