Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa siri ya ushindi kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na serikali kuwa wanapaswa kukifanya chama hicho kuzidi kukubalika ili kiweze kushinda kwa kiwango cha juu uchaguzi Mkuu ujao 2020.

Ameyasema hayo alipokuwa akiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar ambapo amewataka viongozi kutambua umuhimu wao kushuka chini kwa wananchi na kushirikiana nao katika harakati za maendeleo na kubaini changamoto zao ili kuzipatia ufumbuzi na kujenga imani kwa wananchi.

Amesema kuwa viongozi wa Chama na Serikali wana wajibu mkubwa wa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kukiwezesha Chama na Serikali kuendelea kukubalika zaidi kwa  wananchi na kushinda kwa kiwango cha juu zaidi.

Hata hivyo, kikao hicho kilipokea  na kujadili majina ya wagombea 50 waliojitokeza kuomba nafasi za Uenyeviti wa CCM katika Wilaya 12 za Unguja na Pemba na kutoa mapendekezo yake ili kuyapeleka katika vikao husika

Uchaguzi Kenya hati hati kupigwa kalenda
Ferdinand kuingia katika masumbwi