Rais wa Klabu Bingwa nchini Hispania FC Barcelona, Joan Laporta amesema timu yake ni bora kuliko wapinzani wao Real Madrid na inaweza kutwaa tena ubingwa msimu ujao pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Barca walirejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya mapema juma hili na wamesajili wachezaji wawili katika dirisha la uhamisho hadi sasa ambao ni Ilkay Gundogan na Inigo Martinez.

“Tuna timu bora kuliko Madrid na, mchezaji mmoja mmoja, sisi pia ni bora, na tofauti kidogo kuliko wapinzani wetu,” amesema Laporta akiiambia Sport.

“Kama mwanachama na shabiki wa klabu, nimeridhishwa sana na timu tunayoijenga.”

Madrid, ambao walimaliza wakiwa washindi wa pili nyuma ya Barca msimu uliopita wa La Liga, wamewaongeza Jude Bellingham, Joselu, Fran Garcia na Arda Guler.

“Tayari tuna timu yenye ushindani. Tumeshinda Ligi ya Hispania na tunaweza kuendelea kutumia ubabe katika mashindano haya. Pia tunataka kuwa katika kundi la wagombea kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.” amesema Laporta.

“Ninazingatia kuunda timu nzuri juu ya kusajili wachezaji wazuri. Tumewasajili Gundogan na Martinez na watatupa kiwango kizuri kama wengine wanaokuja.

“Tunamkosa beki wa kulia na tunalifanyia kazi. Pia tunataka kuimarisha safu yetu ya kiungo.”

Hata hivyo, Barca walishindwa katika jaribio lao la kumrejesha Lionel Messi katika klabu hiyo katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, huku Mshambuliaji huyo akitimkia Marekani kujiunga na Inter Miami akitokea kwa mabingwa wa Ufaransa PSG.

Mashujaa FC yaanza na Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar
Moalin: Nitaiwezesha KMC FC kuheshimika