Rais Shirikisho la Duniani ‘FIFA’, Gianni Infantino amesema kuwa anataka kuzungumzia mambo mazuri tu wakati wa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake kuhusu tofauti ya malipo kati ya wanaume na wanawake.

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Auckland kuelekea Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake, Infantino pia alitania kuhusu monoloji yake ya ajabu kabla ya Kombe la Dunia la wanaume nchini Qatar.

Novemba, Infantino alisema: “Leo najihisi Qatari, najihisi Mwarabu. Nahisi Mwafrika, nahisi kijana, najihisi mlemavu, najihisi mfanyakazi mhamiaji. Jumatano nilisema najihisi mchovu mara baada ya kuwasili New Zealand. Ni jambo zuri kuwa hapa,” alisema Infantino na kuongeza:

“Kwa wote wanaosubiri kusikia jinsi ninavyojihisi leo…leo nahisi nimechoka kwa sababu ndio kwanza nimetua. Lakini najihisi mwenye furaha sana.

Waandaaji wenza wa Fainali hizo za Kombe la Dunia, New Zealand wenyeji watafungua dimba kwa kucheza dhidi ya Norway kwenye Uwanja wa Eden Park leo Alhamisi (Julai 20) kabla Australia, ambao pia wanaandaa, watacheza dhidi ya Jamhuri ya Ireland huko Sydney baadae leo.

Infantino aliulizwa kuhusu mambo kadhaa yanayolizunguka soka la wanawake. Kikosi cha Australia kilikosolewa kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika zawadi za Kombe la Dunia la wanawake kukosolewa kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika zawadi za fedha katika Kombe la Dunia.

Kwa mara ya kwanza FIFA moja kwa moja itawalipa wachezaji katika Fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake huku kiasi kikiongezeka pale timu inapozidi kusonga mbele.

Kiasi hicho ni kati ya Pauni 24,000 (sawa na Sh milioni 76) kwa mchezaji katika kundi ikiwa ni zaidi ya Pauni 200,000 (sawa na Sh milioni 634), ambazo hutolewa kwa kila bingwa.

Infantino alisema ni jukumu la mashirikisho kuhakikisha fedha zaidi zilizoahidiwa na FIFA wanapewa wachezaji.

“Malipo yoyote tunayofanya, tunafanya kupitia akaunti za mashirikisho ya soka. Na baadaye vyama vya soka hufanya malipo hayo kwa wachezaji wao. Lakini tunashirikiana na vyama vya nchi.

Infantino alitishia kuzizuia TV za Ulaya endapo ofa ya haki za matangazo haitaboreshwa.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) pamoja na ITV walitangaza wiki tano kabla kuwa wamekubaliana na Fifa kutangaza fainali hizo za Kombe la Dunia kwa wanawake.

“Watu wengi wanafikiri kuwa soka la wanawake sio mchezo mkubwa au hauburudishi au ni kuiga soka la wanaume, lakini wakiangalia soka la wanawake kwa mara ya kwanza wataona maajabu na soka lenye kuvutia,” aliongeza.

“Kiwango cha soka la wanawake kimeongezeka katika kipindi cha miaka 10 liyopita.

“Tunataka kuona duniani kote angalau kwa saa moja soka la wanawake linaoneshwa na TV kubwa za nchi kwa sababu hiyo ndio njia pekee ya kuutangaza mchezo.”

Benjamin Mendy apata klabu Ufaransa
Azam FC yafunika kombe Senegal