Rais Joe Biden wa Marekani amekutana na kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis ikiwa ni mara ya kwanza wawili hao kukutana tangu Biden alipochaguliwa kuwa Rais.
Katika mazungumzo yao, wamejadiliana changamoto kuanzia zinazotokana na janga la UVIKO 19 na mabadiliko ya tabianchi na umasikini.
Kwenye mazungumzo hayo, Biden amesifu uongozi wa Papa katika mapambano dhidi ya mzozo wa kimazingira, na namna anavyopigania kuhakikisha kila mmoja anapata chanjo ya corona, pamoja na hatua za usawa za kufufua uchumi ulimwenguni.
Licha ya viongozi hao wanakubaliana katika masuala mengi, lakini wanatofautiana katika mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na haki ya utoaji mimba, ambayo Biden anaiunga mkono, wakati Papa akielezea kuwa ni uuaji.