Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila amesema kuwa ukosoaji unaotolewa na jamii ya kimataifa kuhusu kucheleweshwa kwa uchaguzi katika nchi hiyo si wa kweli.
Ameyasema hayo hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Kinshasa wakati wa maadhimisho ya miaka 17 tangu aingie madarakani, ambapo amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika mwisho wa mwaka huu.
Rais Kabila ameikosoa Monusco huku akisema kuwa ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa hauko nchini DRC ili kuendesha shughuli za taifa hilo.
Aidha, ametoa uhuru kwa kanisa katoliki kufanya maandamano dhidi ya serikali yake, lakini akasema waandaaji wa maandamano hayo ni lazima washtakiwe.
Hata hivyo, Serikali hiyo hivi karibuni ilitangaza kuwa uchaguzi utafanyika tarehe 23 Disemba, ikiwa ni miaka miwili baada ya kukamilika kwa muda wa utawala wa rais huyo.
-
Rais Kenyatta ‘awatuliza’ wanawake
-
Moto wateketeza wagonjwa hospitalini
-
Chuo Kikuu Zimbabwe chaanika ‘Research ya PhD’ ya mke wa Mugabe