Rais wa Rwanda, Paul Kagame ameipongeza Arsenal baada ya Klabu hiyo kuwabanjuwa Manchester City kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 4-1 na kutwaa Ngao ya Jamii kwa mwaka 2023 kwenye Uwanja wa Wembley, juzi Jumapili (Agosti 06).

Arsenal pamoja na kuongoza kwa kipindi kirefu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita, ilijikuta ikiachia ubingwa kwa Manchester City.

Ushindi huo wa juzi utaijenga Arsenal kisaikolojia baada ya kukifunga kikosi cha Pep Guardiola kwa Mikwaju ya Penati baada ya kutoka sare ya 1-1 katika muda wa kawaida na kutwaa Ngao ya Jamii.

Baada ya dakika 70 za mchezo huo wa kuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu England, Cole Palmer aliona kama Man City wameshinda mchezo huo baada ya mchezaji huyo aliyeingia akitokea benchi kufunga bao la kuongoza.

Lakini Leandro Trossard alisawazisha katika dakika ya 101 baada ya shuti lake kubadili mwelekeo na kujaa nyuma ya wavu.

Kufuatia ushindi huo, Rais Kagame ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa Jiji la London, alibuka katika Twitter na kuipongeza Arsenal kwa mchezo huo iliyohitaji kushinda kuelekea msimu mpya.

Msimu mpya wa mwaka 2023/24 wa Ligi Kuu ya England unatarajia kuanza Agosti 11.

“Hongera Arsenal. Inaonesha kile kinachokuja. Unaweza kupenda hicho,” ameandika Rais Kagame.

Rwanda imekuwa mshirika wa Arsenal katika utalii tangu mwaka 2018, ambako timu zote za LigĂ­ Kuu ya England zinavaa “Tembelea Rwanda’ katika mikono ya jezi zao.

Muhogo kuwapa tabasamu Watanzania 600
DPA, Taasisi Elimu ya juu wajielekeza tafiti ukatili wa kijinsia