Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema anarajia kustaafu nafasi yake ya urais aliyohudumu kwa miaka 23 na kwamba matarajio yake baada ya kupumzika ni kuwa Mwandishi wa Habari.
Kagame ameyasema hayo katika kikao na Wanabari baada ya mkutano wake na Rais wa Kenya, William Ruto jijini Kigali na kusisitiza kuwa kustaafu ni hatua isiyoepukika.
Kuhusu mrithi wa nafasi yake Kagame amesema ni jambo linalojadiliwa kikamilifu na Chama Tawala na kwamba si lazima yeye kumchagua mrithi wake bali wataweka mazingira yatakayoleta watu wanaoweza kuongoza
Hata hivyo, maoni ya Kagame yanakuja siku chache baada ya Chama cha Rwandan Patriotic Front – RPF-Inkotanyi, kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa Makamu Mwenyekiti baada ya yeye kukiongoza chama hicho tangu 1998.