Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Desemba 2, 2017 jijini Nairobi, Kenya Rais Karia alipita bila kupingwa kuwa Mjumbe CECAFA.

Awali kinyanganyiro hicho kiliwavutia wanachama wanane kabla ya watatu kujiondoa na hivyo watano hao kuchaguliwa bila kupingwa.

Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa CECAFA, Mhandisi Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kibarua kuboresha utenda kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka ukanda huo.

Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Mwanamke Petra Dorris wa Kenya.

Kilimanjaro Stars kibaruani kesho
DC Bagamoyo awawashia moto waamuzi wa soka wa wilaya