Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia leo Jumatatu (April 25) ametembelea uwanja wa CCM Kirumba na kukagua maendeleo ya ukarabati wake.
Ukarabati wa uwanja CCM Kirumba umeanza mwezi mmoja uliopita ili kuuweka katika ubora unaotakiwa na kukidhi vigezo zinavyohitajika na Shirikisho la Soka Afrika CAF.
Rais Karia amefurahishwa na maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo na kuomba meneja wa uwanja huo Jonathan Nkumba aendelee kumaliza mambo yaliyobaki ili kiwe moja ya uwanja bora nchini Tanzania.
Karia ametembelea eneo la kuchezea (pitch), vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji (dressing room) vyumba vya waamuzi (Refarees room) na kutoa ushauri wa kutengena eneo la Waandishi (Media Atribune) na chumba cha huduma ya kwanza (First Aid).
Meneja wa uwanja huo, Jonathan Nkumba ayakubali maelekezo hayo na kusema kuwa wataongeza nguvu ili marekebisho yote yakamilike kwa muda ili kuruhusu uwanja uanze kutumika.
Karia ameambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza Vedastus Lufano, Katibu msaidizi wa chama cha soka MZFA Khalid Bitebo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF Kelvin Cheela na Mjumbe wa kamati tendaji Malima Kulujirwa.