Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema licha ya kuwa na imani kubwa na Taifa Stars kwenye fainali za Chan, amewataka Watanzania kuacha ushabiki na kukubali uamuzi wa kocha katika uchaguzi wa kikosi kinachopaswa kucheza.

“Mimi naumizwa sana na hii kitu ya ushabiki kwa Watanzania, mtu akiona mchezaji wake anayempenda ndani ya kikosi hayupo basi anaanza minong’ono isiyokuwa na faida, jamani hii ni timu ya taifa kila mchezaji anayepewa nafasi tumwamini.” alisema Karia.

“Mimi nina imani kubwa na timu na Mungu atatusaidia tutafika hata Robo fainali katika michuano hii, muhimu imani hiyo ninayo, basi Watanzania tushirikiane tuache mambo ya kubeza kila kitu, ninaambiwa hata wachezaji huko waliko wana imani kubwa na wanapambana kuhakikisha tinu inafanya vizuri.”

Stars inacheza kesho Jumatano dhidi ya Guinea katika mechi muhimu ya kushinda kuamua nani atasonga mbele kwenye Kundi D.

EAF: Makipa wa kigeni sasa ruhsa kusajiliwa Misri
JPM kuzindua shamba la miti

Comments

comments