Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufanya ziara binafsi ya siku mbili hapa nchini itakayoanza siku ya Ijumaa Julai 5, 2019 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Kenyatta atatua katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita saa 4: 00 asubuhi na kisha kuelekea nyumbani kwa Rais John Pombe Magufuli katika kijiji cha Mlimani wilayani humo.
Aidha, akiwa Chato, Rais Kenyatta atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli.