Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Magufuli, leo Agosti 6, 2020 amechukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Njedengwa Jijini Dodoma.

Zoezi hilo ambalo limeongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijageikiwa ni utekelezaji matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais Magufuli amechukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha pili katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.

Baada ya kuchukua fomu, Rais Magufuli atakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma (White House) ambako atakutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu.

Rais Magufuli achukua Fomu kugombea Urais awamu ya pili

Watalii waendelea kumiminika Tanzania, ndege kubwa zatua na mamia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 6, 2020