Rais dkt. John Magufuli, amemteua Prof. Maurice C.Y Mbago kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) akishika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Amemteua Dkt. Masatu Masinde Leonard Chiguna kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) akichukua nafasi ya Prof. Ninatubu Mbora Lema ambaye uteuzi wake ulitengeliwa na Bodi kuvunjwa.

Aidha, amemteua Prof. Zacharia Mabubu Mganilwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL).

Pia, amemteua Bi. Mariam Alu Nkumbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania huku Dkt. Adam Omar Karia akiteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maji.

Wakati huo huo, Dkt. Godwill George Wanga aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).

Korogwe: Watu wasiojulikana waweka jiwe kwenye barabara ya treni
TCU yafuta vyuo tisa, kimo chuo kikuu na vyuo vikuu vishiriki

Comments

comments