Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24 Februari, 2017 amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. John Kedi Mduma umeanza tarehe 23 Februari, 2017.
Aidha, Dkt. John Kedi Mduma ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Grace Rubambey ambaye amemaliza muda wake.