Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameendelea kufanya teuzi nyingine kama ilivyo utaratibu wake tangu alipoingia madarakani.

Leo Oktoba 19, 2019 amefanya teuzi mbalimbali za viongozi wanne miongoni mwao amemteua Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hashim Abdallah Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea akichukua nafasi ya Rukia Muwango.

Tazama taarifa hapa chini iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa.

IMG_20191019_171730.jpg

Mafanikio ya Taifa Stars yamuibua Haji Manara
Serikali yasema kompyuta zilizoibwa sio za DPP