Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifungua rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa hotuba yake ya kwanza ya mwelekeo wa Taifa leo Novemba 13, 2020 Bungeni jijini Dodoma.

Kabla ya kuanza kuhutubia Bunge la 12 Rais Magufuli aliwaomba wabunge na wageni wote walioko Bungeni kusimama na kutoa ukimya wa dakika moja kuwakumbuka Hayati Benjamin William Mkapa, Rais wa tatu wa Tanzania na wabunge wote walioaga dunia tangu kuvunjwa kwa Bunge la 11.

Akihutubia Bunge, Rais Magufuli ameelezea mipango mbalimbali inayotarajiwa kutekelezwa na serikali yake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumzia suala la kutokuwepo kwa kambi ya upinzani Bungeni, Rais Magufuli amewaonya wabunge kuwa hilo halina maana kuwa wabunge wasikosoe ila wakosoe kwa tija.

 “Kutokuwa Wabunge wa upinzani hatusemi muunge mkono kwenye kila kitu la hasha!, penye kukosoa kosoeni ila mkosoe kwa tija, ” amesema Rais Magufuli.

Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 umemalizika na Spika wa Bunge Job Ndugai ameliahirisha Bunge mpaka Februari 2, 2021.

Gwajima: Rais Magufuli ulikuwa tofali katika ushindi wetu
Ahadi ya Magufuli kwa Rais wa Zanzibar