Rais John Pombe Magufuli amempandisha cheo Kanali Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali baada ya kuridhishwa na utekelezaji wake wa majukumu ya kazi za ujenzi aliyompatia.

Rais ameomba kiundwe kikosi maalumu kwa shughuli za ujenzi ili kisimamie kazi zote za ujenzi na amesema kuwa kikosi hiko kiongozwe na Brigedia Mbuge ambaye amepandishwa cheo leo.

”Kuanzia leo huyu atakuwa Brigedia jenerali kesho kamvishe cheo chake au leo, nimetambua kazi zake ambazo amezifanya” amesema Rais Magufuli.

Aidha Jenerali alipata nafasi ya kuongea amemshukuru sana Rais Magufuli kwa kumpandisha cheo kwani amesema kuwa ni wachache sana wanapandishwa cheo na rais.

Hayo yamefanyika leo jijini Dodoma ambako Rais Magufuli alikuwa anazindua Mji wa Kiserikali Ihumwa.

Pia Rais Magufuli amesisitiza kuwa kuanzia jumatatu ya April 15 wizara zote za Serikali zitatakiwa kuhamia Dodoma kwaajili ya kusogeza karibu huduma za kiserikali kwa wananchi.

LIVE VIDEO: Tafrija ya Kutoa Zawadi kwa Mshindi wa Wimbo Bora wa AFCON2019 U17
Wananchi wafunga ofisi za serikali ya kata

Comments

comments