Rais John Magufuli amemteua Julian Banzi Rafael kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, akichukua nafasi iliyoachwa na Juma Reli ambaye muda wake wa kushika nafasi hiyo ulimalizika Julai 12 mwaka 2015.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imeeleza kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo uliofanywa na Rais umeanza tangu Januari 26 mwaka huu.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Rafael alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

ACT - Wazalendo wairushia rungu CCM, yadai wanataka kusimika utawala wa ‘kiimla’
Serena Williams Ajiwekea Mazingira Ya Kipekee Duniani