Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God limemtunukia tuzo ya heshima Rais John Magufuli ya kutambua mchango wake katika uongozi imara kwa taifa na kwa imani kwa Mungu katika kuliongoza taifa kupambana na janga la Corona.

Askofu Mtakambali amesema kuwa uamuzi wa Rais Magufuli kutokufungia wananchi ndani wakati wa janga la Corona na kuelekeza katika kumtegemea mungu umeliweka taifa kwenye nafasi ya kipekee.

”Uamuzi wako wa kutowafungua watu ndani na badala yake kuwaelekeza wafanye kazi na wamtafute mungu wao kwa bidii ambaye ndiyo jawabu la kweli la mambo yote umeliweka taifa katika nafasi ya peke sana duniani” amesema Askofu Mtakambali

”Katika kumtegemea mungu kwenye medani za kiroho na pia kuliwezesha taifa kutoyumba kiuchumi jambo hili limegusa sana baraza hili tunaomba Mungu akubariki sana na sana kwa kumtanguliza yeye katika uongozi wa taifa letu”amesema Askofu Mtakambali

DC mpya Ilala aapishwa
Mv victoria kuanza kazi jumapili