Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameuagiza uongozi wa Hamashauri ya Ilala kutochangisha fedha katika machinjio ya Vingunguti hadi pale watakapokamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Rais Magufuli amesema hayo, alipofanya ziara ya kushtukiza na kuwataka viongozi wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wengine kuangalia namna ya kukamilisha kazi hiyo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara wa maeneo hayo.

”Kuanzia sasa mkurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine ni marufuku kukusanya mapato ya aina yoyote” amesema Rais Magufuli.

Lakini pia amewataka viongozi hao kufanyia kazi maagizo yake usiku na mchana.

 Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa eneo hilo la machinjioni ambalo linadaiwa kukusanya takribani milioni 100 kwa mwezi.

Hayo yamezungumzwa leo Septemba 16, 2019 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akitokea kwenye uzinduzi wa Rada na kiwanda cha mabomba ya plastiki kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

 

Bondia mtanzania atwaa ubingwa wa A.B.U Afrika Kusini
Mwanafunzi wa shule ya msingi akana kupewa mimba na mkuu wa shule