Rais John Pombe Magufuli leo akiwa kwenye ziara Mkoani Njombe ametaja sababu ya kumtumbua aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani humo.

Ambapo ametaja sababu kuwa ni kushindwa kushughulikia kwa haraka suala la mauaji ya watoto saba mkoani humo.

”Lazima tusimamie kazi zetu, hata hili suala la mauaji yaliyokuwa yanatokea njombe halikutakiwa lichukue muda mrefu hivyo ndio maana RPC wa hapa nimemtoa nimemtoa sababu ameshindwa kusimamia hii kazi” amesema Magufuli.

Amesisitiza kwamba anataka mambo yaende haraka.

Akizungumza hayo Rais Magufuli aliamua kumtumbua na OCD wa mkoa huo lakini mara baada ya mchungaji kuongoza sala ya kuwaombea watoto waliofariki katika mazingira ya kutatanisha na kuwaombea wananchi wa mkoani Njombe kwa mauaji hayo, Rais Magufuli aliamua kumsamehe OCD huyo.

”Na uyo OCD nimemsamehe abaki hapa hapa kutokana na maombi haya” Amesikika akisema Rais Magufuli katika hotuba yake.

Aidha ametoa onyo kali na kusema kuwa endapo tukio hilo likijirudia tena atawaondoa kuanzia mkuu wa mkoa hadi mwenyekiti wa kijiji, hivyo amewataka watu kufanya kazi kwa bidii zote.

”Mkoa wa njombe umepata doa kubwa, siku nyingine yakitokea hayo mkuu wa mkoa unaondoka DED unaondoka, DAS unaondoka, Katibu tarafa unaondoka mpaka Mwenyiki wa kijiji ili kusudi tufike mahali tuwe tunachukua hatua haraka” amesema Rais.

 

 

Rais Magufuli atoa rambirambi milioni 5 mauaji ya watoto Njombe
Mtaa mmoja Marekani kupewa jina la ‘Nipsey Hussle’