Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya uteuzi huo wa Rais iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta wa katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Kaimu Mkurugenzi huyo mpya wa NIDA amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kapilimbi ambaye wiki hii aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

“Uteuzi huo unaanza mara moja,” imeeleza taarifa hiyo.

Picha: Ziara ya Waziri Mkuu Kijiji cha Mtowisa, Rukwa
Serikali kumaliza tatizo la maji Sumbawanga, Rukwa