Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemteua Dkt. Eblate Ernest Mjingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI).

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 29, 2020, na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, na kueleza kuwa Dkt. Mjingo amechukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Simon Mduma, ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mjingo alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Wanyamapori na Huduma za Maabara (TAWIRI),

 Uteuzi huo umeanza leo tarehe 29 septemba 2020

Mikopo inatuchelewesha- Rais Shein
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 29, 2020