Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo Septemba 3, 2018 amefanya uteuzi na kumteua Dk. Antony Kiang’u Jingu kuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kuchukua nafasi ya Bi. Sihaba Nkinga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jingu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Pia Rais Magufuli amemteua Bw. Gabriel Pascal Malata kuwa kamishna wa kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana Ajira na Wenye Ulemavu.

b

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 4, 2018
Video: Hawa ndiyo marais wenye ulinzi mkubwa zaidi duniani