Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Mshtaka DPP, Biswalo Mganga kwenda kuwasikiliza watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi waliopo rumande ili kwa wale walio tayari kutubu ndani ya siku 7 na kulipa fedha walizo hujumu ili waweze kuachiwa huru.

”Kuanzia kesho jumatatu hadi siku ya jumamosi ya wiki inayokuja kama wako watu wa namna hiyo ambao wako mahabusu kwa sababu ya kesi za uhujumu uchumi ambazo zitawafanya wasitoke mapema kwa mujibu wa sheria yetu, lakini wako radhi kurudisha zile fedha na kutubu kwamba hawatarudia, mimi ningeshauri watu wa namna hiyo kama sheria inaruhusu DPP watoke humo ndani” amesema Magufuli.

Ambapo vigogo maarufu walioshtakiwa kwa kesi ya kuhujumu uchumi na kutakatisha fedha ni Wamiliki wa kampuni ya kufufua umeme ya IPTL, Habinder Seth na James Rugemalila, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, Wakurugenzi wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Peter Noni, Rashid Shamtena na Dk Ringo Tenga, Mkurugenzi wa mabasi ya mwendokasi, Robert Kisena, Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania, Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomon, Pia Rais wa shirikisho la soka Tanzania , Jamal Malinzi na wenzake.

Rais Magufuli amezungumza hayo Septemba 22, 2019 akiwa Ikulu jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Rais Magufuli ameongezea kuwa wasipoweza kufanya hivyo ndani ya siku 7 waendelee kubaki mahabusu hata kama kwa miaka 20.

Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa lengo kubwa la kufanya uamuzi huo ni kuwapunguzia uzito wa adhabu watuhumiwa hao lakini pia amesema kama kiongozi ana wajibu wa kusamehe ili kushirikiana pamoja katika kujenga taifa.

 

 

Gianni Infantino kula sahani moja na wabaguzi wa rangi
Fatma Karume ageukia siasa