Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Joseph Pombe Magufuli ameibuka kidedea baada ya kujinyakulia tuzo ya ushindi katika kinyang’anyiro cha Ukombozi wa Afrika mara baada ya mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi Afrika kuonekana.
Ambapo katika Tuzo hiyo ya Ukombozi wa Afrika wamezingatia kipengele cha elimu na Ujinga kama sehemu ya Ukombozi.
Na Tanzania imetolewa mfano kwa hatua iliyofikia ya kutoa elimu bure kutoka shule za msingi mpaka sekondari, na katika suala la umaskini kamati imeangalia hatua ya kuwajali watu wa kipato cha chini ambapo imeangazia hatua ya kuwasajili wafanyabiashara wadogo katika kuwatambua rasmi kwenye shughuli zao na pia kuondolewa kodi za mazao kwa wananchi.
-
Video: Vigogo Chadema wapewa kesi 400, Serikali yamwaga ajira 4,440Video:
-
Mambo muhimu kufahamu endapo unataka kusoma nje ya nchi
Mbali na Tuzo hiyo, Mnamo 2016 Rais Magufuli alishinda tuzo ya Forbes Afrika kwa kuwa mtu anayeheshimika zaidi na aliteuliwa kwa kutambua jitihada zake za kuimarisha uchumi wa Tanzania.
Tuzo ya Ukombozi wa Afrika ni Tuzo zinazotambuliwa barani Afrika na kimataifa likiwa na lengo la kutambua mchango wa viongozi wa bara la Afrika, wapigania Uhuru, wapatanishi wa amani na washiriki wengine wa ukombozi wa Afrika.
Aidha Rais Magufuli anatarajiwa kupokea medali na cheti katika tarehe rasmi itakayotangazwa na kamati baada ya maridhiano kati ya mgeni rasmi na watu w aitifaki.