Rais John Magufuli, leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri aliowateua katika uteuzi wake wa awamu ya pili, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mawaziri na manaibu waziri hao wanaofikia idadi ya watu 6 waliteuliwa na rais Magufuli Desemba 23 mwaka huu na kukamilisha rasmi Baraza la Mawaziri.

Majina ya walioapishwa leo ni yafuatayo:

  1. Prof. Jumanne Maghembe -Waziri wa Maliasili na Utalii.
  2. Dkt. Philip Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
  3. Eng. Gerson Lwenge – Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
  4. Dkt. Joyce Ndalichako – Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
  5. Mh. Hamad Masauni –Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
  6. Prof. Makame Mbarawa –Aliyehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Kafulila Adai NEC Inahujumu Kesi Yake Ya Uchaguzi, NEC Yamruka
CCM Yajipanga Kumpiku Maalim Seif Zanzibar na CUF