Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Jijini Dar es salaam ambapo katika ziara hiyo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema ziara hiyo itaanza Jumatano Februari 24 ambapo Rais Magufuli atazindua Daraja la juu Ubungo (Ubungo interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na Mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis majira ya saa 05:30 asubuhi.

Aidha, Kunenge amesema siku ya Alhamisi ya Februari 25 Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 Asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House ambapo kuna Studio za Channel ten na Uhuru Fm.

Kunenge amesema Ijumaa Februari 26, Rais atafanya shughuli ya uzinduzi wa Nyumba za Polisi na Kiwanda cha kutengeneza sare za Polisi ambapo tukio hilo litafanyika Saa 03:30 asubuhi.

Kocha Sven Vandenbroeck kurudi Tanzania
Julio ajitetea kutolewa AFCON U20