Katika jitihada za kukabiliana na foleni jijini Dar es salaam, leo, Julai 23, 2018 Rais John Pombe Magufuli akishirikiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon watashuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Salender.
Ambapo daraja hilo litaunganisha eneo la Agha-khan na eneo la Coco Beach katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Ture na kutarajiwa kukamilika baada ya miezi 36, na ujenzi utaanza mara tu baada ya mkataba huo wa ujenzi kusainiwa.
Kupitia daraja hili kwa kiasi kikubwa foleni itapungua kwa magari yanayokwenda maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam yakiwemo Msasani, Mwenge, Kinondoni, Masaki, Morocco au Osterbay na maeneo mengineyo yanayopitiwa na barabara hiyo.
-
Video: Lugumi avunja ukimya, Hatuyumbishwi
-
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 23, 2018
Kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikifanya jitahada za kutafuta pesa ili kukamilisha ujenzi huo.
Aidha matangazo hayo yatarushwa moja kwa moja mubashara kupitia runinga na redio ya Taifa, TBC, Lakini pia hapahapa Dar24 tutakuwezesha kufuatilia hatua hiyo muhimu iliyofikwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli.
Pia leo hii Rais, Magufuli anatarajia kupokea gawio la serikali kutoka kwa kampuni, Taasisi, wakala na mashirika ya umma 47 ambayo Serikali in hisa.