Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli, amewashukuru wapinzani kwa kuanza kumpigia kampeni mapema kuelekea katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, kutokana na baadhi ya kauli zao.

Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 6, 2020, katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma, baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa awamu ya pili.

“Mtu akisema nitapigiwa kura na vituo vya afya, najua ndio wameshaanza kunipigia kampeni wao na ninawashukuru sana wanaosema hivyo, maana vituo vya afya wametibiwa wanawake watanipigia kura, Wazee hata walevi walilala humo watanipigia na inanipa nguvu kwamba ushindi wa mwaka huu utakuwa mkubwa,” amesema Rais Magufuli.

“Tulimtanguliza Mungu wakati wa Corona tukafunga siku 3, tukamshukuru siku 3 leo hakuna mwenye Corona hapa tunabanana tu hata Kitandani bananeni tu vizuri, ninasema hivyo kwa sababu aliyenitangulia amesema kampeni tutafanya kitanda kwa kitanda,” amesema Magufuli.

Dkt. Magufuli alipita bila kupingwa katika uchaguzi wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Lebanon yaanza maombolezo ya siku tatu
Rais Magufuli aeleza chanzo cha kujenga ukuta mgodini