Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa, kwa sasa anachukia kuwatumbua viongozi na watendaji wa Serikali lakini anajikuta akichukua uamuzi huo kutokana na baadhi yao kutomuelewa.

“Najaribu kuzungumza hili kwa uwazi ili watu wasije kufikiria mimi napenda sana kutumbua, tena siku hizi sipendi hata kulisikia hilo neno kutumbua, lakini nitafanyaje mtu unamteua pale na hakuna kinachotokea, wengine unaona wanahangaika ila yeye yupo tu, sasa nataka Dkt. Ndumbaro ukafanye kazi.” amesema Rais Magufuli.

Amesema hayo mapema leo Septemba 29, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt. Damas Ndumbaro aliyemteua siku tatu zilizopita.

Rais Magufuli alimteua Dkt. Ndumbaro kuchukua nafasi ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Suzan Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Dkt. Ndumbaro ni mbunge wa Songea Mjini.


EXCLUSIVE: Polepole ataja wabunge wengine 3 Chadema kuhamia CCM “Chadema hawana hata ITIKADI”

Tetemeko lachukua maisha ya mamia
Video: Wamekwisha, Mbunge Chadema ala 'matapishi' yake