Rais wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, kwa kuhusika na mzunguko haramu wa fedha, ufisadi na kumiliki utajiri wenye mashaka.

Abdel Aziz aliiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa muongo mmoja baada ya kuingia madarakani katika mapinduzi ya 2008 na alikuwa mshirika wa nchi za Magharibi, akipambana na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la Sahel. Alikuwa kwenye kesi tangu mwezi Januari na alikanusha madai ya ufisadi.

Mahakama Kuu nchini humo, ilimkuta Abdel Aziz na hatia ya mashtaka mawili kati ya 10 Desemba 4, 2023 kufuatia uchunguzi wa madai ya ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi.

Mmoja wa mawakili wake aliita uamuzi huo ni hukumu ya kisiasa, inayomlenga mtu na familia yake, huku Waendesha mashtaka wa Serikali wakisema hukumu ya mkuu huyo wa zamani wa nchi ilikuwa ya kihistoria.

COP28: Wanawake wafugaji Tanzania wapatiwa tuzo
Picha: Mafuriko Kilosa yalivyosababisha kifo